miss tanzania 2005

 

 

Ushindi wa Nancy Sumari ulileta Faraja na changamoto kubwa kwa wananchi wa Tanzania huku wazazi wakiwahimiza mabinti zao wenye sifa za kushiriki Mashindano ya urembo kufanya hivyo na kuwapa kila aina ya msaada. Huku wazazi hao wakiwa na mategemeo ya mabinti zao kutorudi nyumbani mikono mitupu, kwani wasichana wanaoshiriki katika Mashindano ya urembo pamoja na zawadi ya pesa taslimu baadhi ya washindi wamekuwa wakirudi majumbani na zawadi za Sofa seti, vyombo vya nyumbani kama vile Majokofu, Radio na Luninga za ukubwa mbalimbali, huku wengine wakijishindia magari ya kifahari na wengine kupata kifuta jasho cha nguvu.

 

Kampuni ya simu za mkononi ya REDD'S imeingia Mkataba wa Udhamini wa miaka 5 toka mwaka 2006 hadi 2010 na Kamati inayoandaa Mashindano hayo ya urembo Tanzania . Mkataba ambao pamoja na mambo mengine pia unatoa ajira ya kudumu kwa wasichana hao wanaoshiriki Mashindano hayo ya urembo Nchini Tanzania .

 

 

 

CLick here to advertise

Miss Tanzania 2005 - Nancy Sumari

2005: Katika miaka 10 ya mwanzo ya Mashindano haya toka mwaka 1994 hadi 2004 yalikuwa yakiendeshwa kwa hasara huku Warembo wa Taifa wakijitahidi kufurukuta na kufanya vizuri ili kuibuka washindi katika Mashindano ya Urembo ya Dunia lakini waliambulia patupu hadi mwaka 2005 Miss Tanzania Nancy Sumari aliweka Historia ya Dunia kwa kunyakua Taji la Mrembo wa Dunia, Kanda ya Afrika. [Miss World Africa]

 

Ushindi ambao uliwafurahisha takribani Watanzania wote na kupokelewa na mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, na baadaye kufanyiwa Tafrija kubwa ndani ya viwanja vya Ikulu.

 

Nyota ya Mrembo Nancy Sumari ilianza kung'ara tangu hapa Nchini baada ya kushinda Taji la Mrembo wa kitongoji cha Dar Indian Ocean mshindi wa pili nyuma ya mrembo Natalia Noel. Hata hivyo Mrembo Nancy Sumari hakukata tamaa alijifua zaidi na katika shindano la urembo la Kanda ya Kinondoni Mrembo Nancy Sumari aliweza kunyakua taji la Miss Kinondoni akimuacha mrembo Natalia Noel nyuma yake.

 

Warembo hawa wawili waliweza kuweka historia katika Mashindano ya urembo kwa mwaka 2005 kwani katika ngazi ya taifa mrembo Nancy Sumari alishika nafasi ya kwanza huku Natalia Noel akishika nafasi ya pili.

 

Mrembo Nancy Sumari baada ya kushinda taji la Miss Tanzania alikabidhiwa zawadi kubwa kabisa ya Nyumba ya kisasa yenye kila kitu ndani. [fully furnished] zawadi iliyotolewa na Kampuni ya kutengeneza viatu vya kike ya Ocean Sandals.

 

Kampuni ya Viatu ya Ocean Sandals imeweka rekodi ambayo itadumu kwa muda mrefu kwani hakuna Kampuni nyingine yeyote hadi sasa ambayo imeweza kuvunja rekodi hiyo.

Pamoja na zawadi hiyo ya nyumba yenye kila kitu ndani Mrembo huyo pia alikabidhiwa zawadi ya gari [Saloon] pamoja na pesa taslimu.

 

Mrembo Nancy ambaye aliwakilisha vema nchi yetu katika Mashindano ya urembo ya dunia ambayo kwa mara ya tatu mfululizo yalifanyika tena nchini China , katika kisiwa cha Sanya. Mrembo Nancy ambaye ndege iliyombeba ilichelewa kuwasili nchini huko. Iliwasili majira ya saa 4 usiku kwa saa za huko na kupokelewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Bibi Julia Morley ambaye alianza kumfanyia mahojiano mrembo Nancy Sumari kuanzia muda huo alipowasili na kumpeleka katika hotel waliyofikia warembo wote waliokuwa wakishiriki shindano hilo .

 

Kama hiyo haitoshi, Bibi Julia Morley alimsindikiza mrembo Nancy Sumari hadi katika ukumbi wa chakula [Restaurant] na kufanya mahojiano naye wakiwa pamoja.

 

Si hivyo tu, bali ushindi wa Nancy Sumari katika Mashindano ya urembo ya dunia, ulitokana na juhudi zake katika kushindana katika michezo mbalimbali kama vile kuogelea, kuvuta kamba, kuruka vihunzi, kujibu maswali n.k.

 

Mrembo Nancy Sumari mara baada ya kurejea nchini akitokea huko Sanya China na kuandaliwa Tafrija kubwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Mrembo Nancy Sumari alikabidhiwa zawadi ya Vito vya thamani, pamoja na kupata Mikataba mbalimbali ndani na nje ya Nchi.

 

Mrembo Nancy Sumari kwa sasa anasubiri kujiunga katika Chuo Kikuu cha Nairobi Kenya kwa Masomo ya Shahada ya Sheria.